>WENGINE WAWILI WAUAWA NDANI YA NYUMBA KISHA KUCHOMWA MOTO.
MWANAMKE mmoja wa kijiji cha Mwaoga-Makongorosi, amekufa papo hapo baada ya kukatwa katwa mapanga na mwanaume ambaye naye alikamatwa na wananchi wenye hasira kali na kuuawa.
Tukio hilo la aina yake linalodaiwa chanzo ni wivu wa kimapenzi, limetokea jana saa 7:40 mchana, katika kijiji hicho kilichopo wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa polisi mkoani hapa, Monica Madembwe, alisema kuwa marehemu wote wawili hawajaweza kufahamika majina ya.
Monica alisema kuwa mwanamke huyo mwenye umri kati ya miaka 30-35, akiwa katika barabara ya Mkwajuni kwenda Makongorosi, alishambuliwa na mwanaume huyo mwenye umri kati ya miaka 20-25 kwa kukatwa katwa mapanga na kufariki papo hapo.
Kaimu Kamanda Monica alisema baada ya kufanya mauaji hayo, wananchi wenye hasira kali walimkamata na kumshambulia kwa mawe, fimbo na marungu hadi na yeye kufariki.
Aliongeza kuwa hakuna mtu ama watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo, ambalo chake chake inasadikiwa ni wivu wa kimapenzi.Uchunguzi zaidi unaendelea.
Katika tukio lingine lilitokea kijiji cha Itimba-Utengule wilaya ya Mbeya vijijini, watu wawili wameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani wakiwa ndani ya nyumba yao.
Monica aliwataja marehemu hao kuwa ni Merry Mpenzu (50) na William Mpenzu (30).
Akielezea zaidi tukio hilo, alisema marehemu hao wawili wakiwa ndani ya nyumba walivamiwa na watu wasiofahamika na kupigwa na kitu kizito vichwani, kufungiwa mlango na baadaye nyumba hiyo kuwashwa moto.
"Nyumba yao ilikuwa imeeezekwa kwa nyasi, hivyo baada ya marehemu hao kuuawa, wauaji hao waliezua paa la nyumba hiyo na kulitumia kuchoma moto nyumba hiyo huku marehemu hao wakiwa ndani" alisema Monica.
Uchunguzi zaidi kujua chanzo cha mauaji hayo pamoja na kuwasaka watuhumiwa unaendelea kufanywa.Wakati huo huo mkazi wa kijiji cha Hatelele, wilayani Mbozi ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kikali kichwani.
Marehemu ametajwa kuwa ni Evance Halele (29), ambaye mwili wake ulikutwa umetupwa kwenye mtaro wa barabara.
Imedaiwa kuwa marehemu alikuwa anajishughulisha na matukio ya wizi na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Tuesday, June 16, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment