Friday, June 19, 2009

MTIKISIKO WA YUCHUMI DUNIANI

KATIKA hatua muhimu ya kudhibiti huduma za benki nchini Marekani, Rais Barack Obama ametangaza sera mpya zenye lengo la kuhakikisha msukosuko wa kifedha ulioikumba nchi hiyo hautokei tena.

Kufuatia mabadiliko hayo, benki zilizostawi zitahitajika kukuza hazina ambayo itatumiwa kukabiliana na hasara zozote.

Pia kutabuniwa shirika maalum la kutetea haki za wateja ikiwa ni pamoja na kusimamia mfumo wa rehani na mikopo.

Rais Obama aliyataja mabadiliko hayo kuwa ndiyo muhimu zaidi kuwahi kubuniwa katika mfumo wa fedha nchini Marekani tangu miaka ya 1930.

Benki kuu itasimamia utekelezaji wa mabadiliko na imepewa mamlaka ya kuchunguza mienendo ya taasisi za kifedha na benki.

Rais Obama alisema makampuni mengi pamoja na wateja wamepata hasara kubwa kutokana na kutokuwepo na sera mufti za kusimamia benki.

"Tunafanya kila tuwezalo kujenga msingi thabiti wa kukuza uchumi kwa njia endelevu. Hili halitakuwa jambo rahisi" alisema Rais Obama.

No comments:

Post a Comment