SHIRIKA la Afya Duniani (WHO),limetoa msaada wa friji kumi za kuhifadhia damu kwa Tanzania, kutokana na mafanikio makubwa yaliyoyafikiwa kwa muda mfupi tangu mpango wa damu salama uanzishwe mwaka 2005.
Imeelezwa kuwa hatua hiyo ya WHO ni kuichangia mpango wa damu salama nchini.
Hayo yamo katika salamu za Mkurugenzi wa shirika hilo,barani Afrika Dk.Luis Gomes Sambo, zilizotolewa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kuchangia damu duniani, ambapo kitaifa ilifanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini mbeya.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaliyotanguliwa na maandamano kutoka kituo cha mafuta Oil Com kilichopo Soweto hadi katika viwanja hivyo, alikuwa ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa.
Sambo alisema kuwa tunaposherehekea na kuwatambua wachangia damu kwa hiyari, kwa ‘zawadi ya uhai’ ni muhimu kukumbuka kuwa ongezeko la wachangiaji damu hao mara kwa mara ndio njia pekee ya kuhakikisha upatikanaji wa damu salama kwa kila mgonjwa.Mkurugenzi huyo wa WHO barani afrika alisema:
”Mahitaji ya damu barani Afrika yanaongozwa na tatizo la vifo vya kina mama hadi kufikia elfu moja ambapo kwa watoto laki moja wanaozaliwa hai, zaidi ya asilimia 40 ya vifo vyao husababishwa na kutokwa damu”.
Aliongeza kuwa inakadiriwa kuwa asilimia 90 ya vifo milioni moja kila mwaka duniani kote, kutokana na ugonjwa wa maralia hutokea katika bara la afrika wakati kwa sehemu nyingine vifo hivyo vinavyotokana na maralia kali na ukosefu wa damu hufikia hadi asilimia saba na nusu.Dk.
Sambo alisema WHO limeunda mkakati wa damu salama mnamo mwaka 2001 nia ikiwa ni kulenga utoshelevu pamoja na usalama wa damu na tangu wakati huo kumekuwa na maendeleo mazuri katika kukusanya na kupima damu pia kuzuia magonjwa yanayoenea kwa damu.
“Lengo mojawapo katika mkakati huu ni kila nchi iweze kuchangia kwa hiari sio chini ya asilimia 80 ya mahitaji yake ya damu ifikapo mwaka 2012” alisema Dk.Sambo.
Aliongeza kuwa zaidi ya asilimia 50 ya nchi wanachama wamefikia lengo hilo ambapo nchi kumi na mbili kati ya 46 hukusanya damu yote inayohitajika kutoka kwa wachangia damu kwa hiari.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, zaidi ya lita milioni 3.2 ya damu inakusanywa barani humu ila hata hivyo kuna upungufu kutokana na mahitaji ya lita milioni nane kwa mwaka hivyo juhudi zaidi zinahitajika ili kufikia lengo hilo.
Naye Meneja wa Mpango wa Damu salama nchini, Efespar Nkya,alisema hapo awali kulikuwa hakuna mfumo uliokuwa ukisimamia na kuratibu huduma za upatikanaji na upimaji damu uliokuwa ukizingatia ubora wa viwango.
Nkya alisema mfumo huu unategemea wachangiaji ndugu,marafiki na wakati mwingine watu wanaolipwa na kuwa mfumo huo una kiwango kiwango kikubwa cha maambukizi ya magonjwa kupitia kwenye damu, upungufu wa damu mara kwa mara na kukosekana.
Tuesday, June 16, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment