Monday, July 27, 2009

MARY MWANJELWA AKITOA MSAADA WA SHATI ZA CCM

MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa, Mary Mwanjelwa akimkabidhi Katibu wa UWT wilaya ya Mbeya mjini, Sarah Mgoli, msaada wa shati zenye nembo ya CCM kwa ajili ya wajumbe wa Baraza la UWT wilayani humo.

KIKUNDI cha Uhamasishaji cha CCM kutoka kata ya Maanga, jijini Mbeya, kikitoa burudani kwa wajumbe wa Baraza la UWT wilaya ya Mbeya mjini, katika kikao kilichohutubiwa na Mary Mwanjelwa

MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa, Mary Mwanjelwa (kushoto), akitoa msaada wa kadi 100 za UWT kwa Katibu wa jumuia hiyo wilaya ya Mbeya vijijini, Mgeni Ottoh.



MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Mbeya vijijini, William Simwali, akimshukuru Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa, Mary Mwanjelwa, mara alipotembelea ofisi za Chama na kutoa msaada wa sh.50,000 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa jengo hilo ambao bado unaendelea.




BASI la kampuni ya Mabruku lenye namba za usajili T.495 AAV aina ya Scania lifanyalo safari zake kutoka Mbeya kwenda wilayani Chunya, likiwa limepata ajali katika eneo la Charangwa nje kidogo ya Chunya hata hivyo hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo.




No comments:

Post a Comment