MKAGUZI wa mazao ya kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Damian Gasana, amewataka wananchi wa mikoa ya kanda za juu kusini, kutoa taarifa na kuorodhesha viuatilifu chakavu.
Alisema viuatilifu hivyo ambavyo vina athari kwa binadamu na mazingira vitakusanywa na watalaamu maalumu.
Gasana alisema kipindi cha mwaka 1997/1998, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), lilifanya tathimini na kubaini kuwepo kwa tani 1,000 za viuatilifu na tani nyingine 200 za madawa ya chakavu ya mifugo.Taka hizo zimeonekana katika maeneo yasiyopungua 325 nchini kote.
Hayo aliyasema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mradi wa Africa Stockpiles ambao una mkakati wa kukusanya viuatilifu hivyo kwa mikoa ya kanda hii.
Gasana wananchi wote wanawajibika kutoa taarifa sahihi za uwepo wa viuatilifu chakavu kwa mabwana shamba na ofisi ya kilimo ya wilaya ambapo alisema kuwa wananchi hawatakiwi kushika wala kuhamisha viuatirifu na kwamba kazi hiyo itafanywa na wataalamu maalumu waliofundishwa.
Alisema kuwa shughuli ya kutoa taarifa kuhusu viuatilifuy chakavu ni hiyari na kwamba hakuna hatua zozote za kisheria zitakazochukuliwa kwa wananchi watakaotoa taarifa juu ya uwepo wa viuatilifu, “viuatilifu ni neon linalotumika badala ya neno la dawa za kilimo”.
Alivitaja baada ya viuatilifu chakavu kuwa ni vyote vilivyoisha muda wake, vilivyopigwa marufuku kutumika nchini kisheria, bidhaa za viuatirifu zilizopondeka na kuharibika pamoja na vyombo au vitu vilivyoathirika au kuchafuliwa na viatilifu hivyo.
Aidha, Gasana alisema kuwa hiyo nafasi pekee ya kuisafisha nchi kuondokana na sumu zilizolundikana ambapo alisema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kushiriki kutoa taarifa ili viatilifu hivyo viondolewe katika makazi ya wananchi pamoja na kuondokana na vyanzo vya uharibifu wa mazingira.
Sunday, July 19, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment