KATIBU Tawala Msaidizi wa mkoa wa Mbeya, Moses Chitama, amesema kuwa asilimia 18 ya watumishi 402 wa ofisi ya Mkuu wa mkoa Mbeya, wamekutwa na virusi vya ugonjwa wa Ukimwi.
Chitama alisema kuwa upimaji huo wa hiyari ulifanyika mwaka 2004 na majibu yake yalitolewa hivi karibuni na kubainika idadi hiyo ya watumishi kuwa wameathirika na ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa waraka uliotolewa na serikali ni kuwa watumishi wote wanaopimwa afya zao na kukutwa na virusi vya Ukimwi, ofisi husika huwa inawahudumia mambo mbalimbali ikiwemo posho kwa ajili ya kuwawezesha kupata lishe bora na usafiri wa kwenda na kurudi kwenye matibabu.
Alisema hivyo ni vyema watumishi wengine wajitokeze kupima afya zao ili waweze kujitambua kwani hivi sasa dawa za kurefusha maisha ARV'S zinatolewa bure hivyo hawana haja ya kuogopa kujitokeza.
Friday, May 15, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment