SERIKALI mkoa wa Mbeya, imeuagiza uongozi wa halmashauri ya jiji la Mbeya, kutomkamilisha malipo mkandarasi aliyejenga barabara inayoanzia benki ya Stanbic, kuelekea Ikulu ndogo kwani imejengwa chini ya kiwango.Imeelezwa kuwa hadi sasa halmashauri tayari imemlipa Mkandarasi huyo shilingi milioni 43 kati ya milioni 132 anazotakiwa kulipwa kwa kazi hiyo.
Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya,John Mwakipesile, kufuatia malalamiko yaliyofikishwa ofisini kwake na wananchi wa eneo la Uzunguni,inapopita barabara hiyo kufuatia adha ya vumbi wanayoipata wakati barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami.
Mwakipesile alisema kuwa hata yeye kiwango cha utengenezaji wa barabara hiyo kilimtia mashaka,hali iliyopelekea kumuagiza mtaalamu kutoka Wakala wa barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mbeya kwenda kuifanyia ukaguzi ili kuona kama imejengwa kwa kiwango.
"Mtaalam niliyemtuma kutoka TANROADS aliikagua barabara hiyo na kubaini kuwa imejengwa chini ya kiwango kinachotakiwa...hivyo naagiza kuwa mkandarasi huyo asilipwe fedha zilizobaki hadi tujiridhishe na kazi iliyofanyika" alisema Mwakipesile.
Aliongeza kuwa wakazi wa eneo la Uzunguni wamekuwa wanampelelekea malalamiko kutokana na adha ya vumbi linalotimka katika barabara hiyo ambayo ilitakiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.
Friday, May 29, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment