BARABARA zenye urefu wa kilometa 30, zinatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami, katika halmashauri ya jiji la Mbeya, baada ya jiji hilo kuingizwa katika mpango wa Benki ya Dunia (WB), wa kuboresha miundombinu.
Sambamba na hilo, benki ya Dunia kupitia mradi huo ilikubaliana na jiji la Mbeya, kuiongezea uwezo wa kukusanya mapato yake yenyewe.Gharama za mradi wote zinatarajiwa kuwa shilingi bilioni 21.
Kaimu Mhandisi wa jiji la Mbeya, Masalu Bashiganye, akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema kuwa mwishoni mwa mwaka uliopita, jiji lilibahatika kuingizwa kwenye mpango wa benki ya Dunia wa kuboresha miuondombinu yake.
Alisema kuwa mradi huo utahusisha ujenzi wa barabara, kwa kiwango cha lami katika stendi ya Nanenane na pia kuboresha usafi, kwa kununua magari kwa ajili ya kuzolea takataka.
"Utekelezaji wa mradi huu utachukua muda wa miaka mitatu na utafanyika katika awamu mbili tofauti kuanzia mwezi Machi,mwakani" alisema Bashiganye.
Aliongeza kuwa hivi sasa jiji la Mbeya, linaendelea na michakatoi mbalimbali kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI na Benki ya Dunia, ili kuwapata Makandarasi washauri.
Bashiganye alisema Makandarasi hao ndio watakuwa na kazi ya kubuni ama kussanifu miundombinu hiyo na kutengeneza nyaraka za zabuni ambazo ndizo zitatumika kuwapata makandarasi wa kujenga miundombinu hiyo.
Kaimu Mhandisi alisema mchakato huo unaendelea na unatarajia kukamilika mapema mwakani na halmashauri katika mradi huo itachangia wataalamu wa usimamizi katika ujenzi kwa maeneo mbalimbali.
Aliwataja wataalamu hao kuwa ni kutoka idara mbalimbali zikiwemo ya Ujenzi, Afya, Utumishi, Fedha na uthamini wa mali na ile ya Maendeleo ya Jamii.
Pia Kitengo cha Uthamini kitashirikishwa katika kuthamini nyumba mbalimbali za jiji la Mbeya, ambazo bado hazijafanyiwa uthamini ili zianze kulipiwa kodi ya majengo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nice post. Thank you for the info. Keep it up.
ReplyDelete