OFISA Kilimo wa wilaya ya Rungwe, Faya Ilanga, amesema halmashauri ya wilaya hiyo imetenga shilingi milioni 800, kwa ajili ya shughuli za kilimo wilayani.
Katika kiasi hicho cha fedha, shilingi milioni 23 zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza zao la Mananasi ili kuwakomboa wakulima wazalishaji wa matunda hayo, ambao hawana soko la uhakika.
Ilanga aliyasema hayo alipokuwa akizungumzia kuhusu matatizo yanayowakabiri wakulima pamoja na mikakati iliyopo ili kuhakikisha kilimo kinaboreshwa wilayani humo.
“Tatizo kubwa tulilonalo ni kwamba wakulima wengi wa matunda hawana elimu ya utafutaji masoko…pia ukosefu wa viwanda vya kusindika matunda hayo.Lakini iwapo wadau wa kilimo wataungana,shughuli za kilimo zitakuwa na manufaa makubwa” alisema Ilanga.
0000
Wednesday, May 20, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment