Wednesday, May 20, 2009

MEYA JIJI LA MBEYA AMPINGA MKURUGENZI

MEYA wa halmashauri ya jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, amepinga kauli iliyotolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa jiji, Elizabeth Munuo kuwa, amefanya juhudi binafsi kuagiza magali mawili kwa ajili ya kuzoa takataka.
Jiji la Mbeya ambalo lipo mipaka inayoiunganisha nchi ya Tanzania na nchi jirani za Malawi, Zambia, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hivi sasa linanuka kwa uchafu uliokithiri.
Hivi kufuatia kero hiyo, hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, alimtaka Mkurugenzi Elizabeth, kutafuta kituo kingine cha kufanyia kazi iwapo ameshindwa kuondoa uchafu jijini Mbeya.
Hatua hiyo ya Mwakipesile ilifuatia Elizabeth akiwa katika kikao kimoja kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benjamin Mkapa, kutakiwa kutoa sababu zinazopelekea jiji kukithiri kwa uchafu, alijibu kuwa amechoshwa majungu ya wakazi wa jiji la Mbeya.
Alibainisha kuwa maeneo yote aliyoteuliwa kufanya kazi ameweza kufanya vizuri, lakini hali imekuwa tofauti kwa Mbeya, hivyo anajuta kuhamia jijini hapa.
Kauli hiyo iliwakera wajumbe wengi wakiwemo Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya, Hilda Ngoye na Mwenyekiti wa halmashauri ya ya Rungwe, John Mwankenja kumtaka arekebishe kauli yake.
Hivyo Meya Kapunga alisema kuwa Madiwani katika kikao walichokaa, walikubaliana kwa kauli moja kuidhinisha kiasi cha kasma ili kiweze kutumika kuyafanyia marekebisho magari ya kuzoa taka.

"Ni kweli Jiji la Mbeya hivi sasa ni chafu...Mbeya inarudi nyuma badala ya kwenda mbele kutokana na mambo yetu sisi wenyewe" alisema Kapunga.

Kapunga aliongeza kuwa Baraza la Madiwani lilikubali kuidhnisha kasma ya fedha ili kukabiriana na kero ya ongezeko la uchafu jijini hapa, lakini inaonyesha kuwa hilo halijaweza kufanyiwa kazi.

Meya alisema kiasi hicho kilikuwa ni kwa ajili ya kufufua magari ya uzoaji taka na kuhakikisha kuwa magari hayo yanapatiwa mafuta mapema ili yaanze kazi ya kusoma taka mapema.

Aidha, alisema kuwa ni hili kukabiriana hali hiyo ya uchafu uongozi wa jiji uliamua maghuba yote yaliyokuwa pembeni ya barabara kuu yaondolewe na kuweka katika barabara ambazo zipo ndani ili kupunguza kero hiyo machoni mwa wageni wakiwemo viongozi wakuu wa kitaifa, wakati juhudi za kupata ufumbuzi wa kudumu zinaendelea.

"Lakini hii kampuni tuliyoipa kazi ya kutuletea magari hayo hadi leo haijaweza kufanya hivyo...tutamdai fidia ili aweze kutulipa fedha kwa ucheleweshaji huu kwani tuliingia naye mkataba" alisema Kapunga.

0000

No comments:

Post a Comment