
WAUZAJI wa ndizi katika soko la Tandale, lililopo mji wa Kiwira wilayani Rungwe wakiendelea na biashara kama kawaida.

MWANAFUNZI huyu wakati wenzake wakiendelea na masomo darasani, yeye hilo halitambui anaendelea kusaka sheli kwa kuosha magari jirani na ofisi kuu za Posta, jijini Mbeya. Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Leonidas Gama, amemtaka Mkuu wa polisi wilaya, kuhakikisha kuwa watoto hawa hawaendelei na kazi hiyo, bali wanarejea shule kuendelea na masomo.Elimu ni ufunguo wa maisha, vijana fedha mtazikuta tu.

WANACHAMA wa saccos ya Bonde la Uyole ambayo ni moja ya saccos ya mfano nchini kutokana na hatua kubwa waliyofikia wakiwa na mtaji wa zaidi ya shilingi bilioni mbili.Tukipata saccos nyingi kama hizi dhana ya Maisha bora kwa Watanzania itafikiwa bila kikwazo.

HAPA ni soko la Tandale,lililopo Kiwira wilayani Rungwe, mkoa wa Mbeya.

MADIWANI wa halmashauri ya jiji la Mbeya, wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment