MARY Kagali (19), ameshinda taji la Miss Mbeya 2009, baada ya kuwashinda warembo wengine kumi na mmoja waliojitokeza kuwania taji hilo na kujinyakulia zawadi ya sh.800,000.
Shindano hilo, liliingia dosari baada ya kiongozi wa majaji,Tasha Jim kumtangaza mrembo, Raulensia Laurency kuwa mshindi namba mbili, hali iliyopelekea ukumbi mzima kuzomea kupinga matokeo hayo.
Mamia ya mashabiki lukuki waliohudhuria shindano hilo, lililofanyikia katika ukumbi wa Benjamin Mkapa, walifikia hatua hiyo baada ya Raulensia kushindwa kuonyesha uwezo katika kutembea pia kwenye kujibu swali ili kumpima ufahamu wake.
Kwa kushinda nafasi hiyo, mrembo huyo alijinyakulia zawadi ya shilingi 400,000 huku nafasi ya tatu ikitwalia na Agnes Mpona, aliyezawadiwa shilingi 200,000.
Warembo hao watatu wataungana na mrembo aliyeshika ya nne, Jacqueline Magayane kuingia katika shindano la kumsaka mrembo wa kanda ya nyanda za juu kusini.
Awali warembo hao kumi na wawili walipita jukwaani na kuonyesha mavazi ya ubunifu, ufukweni na baadaye kumaliza na vazi la kutokea jioni, ambapo walichujwa na kupatikana tano bora.
Waliofanikiwa kuingia tano ni Jacqueline Magayane, Neema Mushi, Agnes Sasawata, Raulensia Laurency na Mary Kagali ambaye kila alipokuwa akipita jukwaani ukumbi mzima ulikuwa unalipuka kwa kofi na mayowe kumshangilia.
Mashabiki wa shindano hilo, walimtupia lawama jaji mkuu, Tasha Jim, kwa kuharibu shindano hilo kufuatia kumtangaza Raulensia kuwa mshindi wa pili ambaye wengi waliona kuwa hakustahili kutwaa nafasi hiyo.
Shindano hilo, lilipambwa na burudani kutoka kikundi cha muziki wa taarabu cha Victoria Modern kutoka Dar es Salaam lenye wasani wa kike watupu pamoja na kundi la muziki kutoka jijini Mbeya lililo chini ya msanii Robby Matunda.
Saturday, May 30, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment