CHAMA cha mpira wa kikapu mkoa wa Mbeya, kimesema kuwa hakiwezi kushiriki mashindano ya klabu bingwa ya mchezo huo, yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza, hivi karibuni.
Imeelezwa kuwa ni vyema TBF liwe linaweka mashindano hayo katika mikoa ya iliyo katikati ili timu nyingi zaidi ziweze kushiriki, kwani kutoka Mbeya mkoa uliopo kanda ya nyanda za juu kusini hadi kufika Mwanza ni vigumu kwa timu ya mkoa iitwayo Mbeya Flames kuweza kushiriki.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Chama cha Mpira wa kikapu mkoa wa Mbeya, Yusuph Nyirenda, ambap alisema kuwa kuipeleka timu hadi Mwanza ni gharama kubwa ambayo hawawezi kuimudu.
ooooo
Wednesday, May 20, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment