WAJUMBE wa kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Mbeya, wamemuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa kuhakikisha kuwa bajeti ya barabara inayotakiwa kupitishwa inapitiwa kwanza na kikao hicho.
Imeelezwa kuwa TANROADS wamekuwa wanapitisha bajeti hiyo na kuamua wao barabara za kuzitengeneza badala ya zile zinazotakiwa na wananchi wa wilaya husika.
Wakichangia katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika jana.chini ya Uenyekiti wa Mkuu wa mkoa wa Mbeya,wajumbe hao walisema kuwa barabara zinazotengenezwa na TANROADS zinatakiwa kujibu kero za wananchi na siyo nje ya hapo.
Walisema kuwa hivyo kuanzia bajeti ijayo ni lazima kabla ya kupitishwa iwe inaletwa kwenye kikao hicho kujadiriwa ili barabara zitakazotengenezwa ziwe ni zile zinazopewa kipaumbele na wananchi na siyo wakala huyo wa barabara.
“Ni vyema hili lifanyiwe kazi ili barabara zile zinazotakiwa na wananchi kutokana na umuhimu wake ndizo zipewe kipaumbele cha kwanza na siyo zile ambazo TANROADS mmekuwa mnaziamua na kuzipangia bajeti bila ya kutushirikisha” walisema.
Friday, May 29, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment