MEYA wa halmashauri ya jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, amechaguliwa kwa kishindo kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, wilaya ya Mbeya mjini baada ya kuwabwaga wagombea wengine wawili walijitokeza.
Kapunga alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 122 na kuwashinda wapinzani wake, Sure Mwasanguti aliyepata kura 60 huku Mwajuma Tindwa, ambaye alikuwepo nje ya ukumbi na kuingia 'mitini' dakika za mwisho akiambulia kura 3.
Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari iliyo chini ya Jumuia ya Wazazi ya CCM, Sangu iliyopo mjini hapa,ulihudhuriwa na wajumbe 187 wa halmashauri Kuu ya CCM wilaya hiyo.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Ernest Machunda, alipowataka wajumbe kufanya zoezi kla kuhakiki> wajumbe halali wa mkutano huo.
Katika hali ya kushangaza, wajumbe kutoka kata ya Mwasanga, walilazimika kupitishwa mbele ili kuhakikiwa ambapo ilibainika mjumbe mmoja, Amani Salone, ambaye alijitambulisha kama Kaimu Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo, kubainika kuwa siyo mjumbe.
Machunda alilazimika kumtoa nje Salone na ndipo wagombea walipoanza kujieleza akianza Kapunga, Mwasanaguti na Katibu wa CCM wilaya, Bahati Makalanzi, alilazimika kusimama na kumuombea kura Mwajuma.
Akiomba kura Kapunga aliwaomba wajumbe kumchagua kushika nafasi hiyo kwani anao uzoefu na nafasi hiyo ambayo alisema aliwahi kuiongoza katika vuipindi tofauti.
"Nimeifanya kazi hii ya Uenezi katika kvipindi viwili tofauti na nilifanikiwa kwa kushirikiana na wana-CCM wilaya hii, kuweza kulirudisha jimbo hili ambalo lilikuwa linashikiliwa na Polisya Mwaisyeje wa chama cha upinzani cha> NCCR-Mageuzi.
Mara baada ya matokeo kutangazwa na Kapunga, kupatikana mshindi, ukumbi ulilipuka kwa shangwe na kuimba nyimbo za Chama, hali iliyoashiria kuwa wajumbe waliridhika na matokeo hayo.
Kwa upande wake Mwasanguti aliwashukuru wajumbe wa kikao hicho kwa kupata kura 60, na kuongeza kuwa hizo si haba kwani hiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuomba kura kwa wajumbe wa kikao hicho.
Awali Mwasanguti alikuwa ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Mbeya mjini, na alistaafu baada ya umri wake kutomruhusu kugombea tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
0000
Tuesday, May 26, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment