ASKARI wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA), kambi ya Nyota wilayani Mbarali, mwenye cheo cha Staff Sajenti, Brighton Ng’umbi (57), ameuawa na watu wasiojulikana na maiti yake kutupwa katika mfereji wa maji.
Mwili wa marehemu Ng’umbi ambaye alipotea tangu Mei 23,mwaka huu saa 5:00 usiku, akitokea katika baa ya Oasis iliyopo Rujewa, ulikutwa katika mfereji huo unaosafirisha maji kwenye mashamba ya mpunga ya kampuni ya Highland Estate Ltd.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen, alisema mwili huo uliokotwa jana saa 2:00 asuubuhi ukiwa umetupwa katika mfereji huo.
Stephen alisema uchunguzi uliofanywa kwenye mwili wa marehemu Ng’umbi umeonyesha majeraha kwenye paji lake la uso na mdomoni.
“Polisi inamshikilia Rebecca Emmanuel (39), maarufu zaidi kwa jina la Mwakyami, mkazi wa kijiji cha Ihango, kwa tuhuma za kuhusika na kifo hicho” alisema Stephen.
Alifafanua kuwa mtuhumiwa Rebecca ametiwa mbaroni kwani ndiye alikuwa na marehemu siku ya mwisho kabla ya kutoweka wakiwa wanakunywa vinywaji katika baa hiyo ya Oasis, hivyo anaisadia polisi.
Alisema uchunguzi zaidi ili kuwabaini watuhumiwa waliohusika na mauaji ya askari huyo wa doria wa TANAPA (Park Ranger), unaendelea kufanywa na polisi.
Thursday, May 28, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment