OFISA Kilimo mkoa wa Mbeya, Grace Ngwassy, amesema biashara ya mahindi mabichi inayofanywa na baadhi ya wakulima wilayani Rungwe, haiwezi kusababisha baa la njaa kwani haina athari.
Alisema kuwa wamewasiliana na wataalamu wa kilimo wilaya ya Rungwe, kuhusu suala hilo na wamehakikisha kuwa biashara hiyo haiwezi kusababisha njaa kwa upande wa wilaya na mkoa kwa jumla.
Grace aliyasema hayo alipotakiwa kutoa msimamo wa serikali mkoa ili kujua wamechukua tahadhari zipi kutokana na kushamiri kwa biasahara ya mahindi mabichi wilayani Rungwe.
“Hakutakuwa na athari kwa ipatikanaji wa chakula mkoani hapa kufuatisa biashara hiyo, kwani tumefanya utafiti kwa kuwatumia wataalamu wetu wa kilimo wilaya ya Rungwe na wametuhakikishia hilo” alisema Grace.
Ofisa Kilimo alisema serikali mkoa haihalalishi biashara hiyo ya uuzaji mahindi mabichi yakiwa bado shambani, lakini imeamua kufanya hivyo ili kumuwezesha mkulima aweze kufidia gharama za kilimo.
Grace alisema mkulima anatakiwa apate fedha za kuweza kujikimu na kununua pembejeo za kilimo, hivyo kwa wilaya ya Rungwe wakulima wanao utaratibu wa kutenga maeneo ya mashamba kwa ajili ya mahindi mabichi ambayo huyauza na maeneo ya mashamba yaliyobaki hulima kwa ajili ya kuja kupata mavuno ya chakula na ziada huwa wanauza kwa wafanyabiashara.
Aliongeza kuwa katika utafiti walioufanya wameweza kubaini kwamba biashara hiyo haijaweza kufikia kiwango cha kutishia usalama wa chakula kwa wilaya husika na mkoa wa Mbeya.
“Lakini vile vile ukiangalia utabaini kuwa biashara hii ya mahindi mabichi ni ya msimu tu, hivyo msimu wake ukimalizika nayo huwa imeisha…nia ya serikali ni kumkomboa mkulima ili kilimo kiweze kumpatia tija” alisema Grace.
Baadhi ya maeneo yaliyokithiri kwa biashara hiyo ni Ndaga, Isyonje na Ntokela ambapo wakulima wengi wamekuwa wanakusanya mahindi na kuyaweka pembezoni mwa barabara kwa ajili ya kutafuta wateja wa kuyanunua.
0000000
Wednesday, May 20, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment